Mtalii mmoja raia wa Ujerumani aliyekua akitibiwa ugonjwa wa COVID-9 unaosababishwa na virusi vya corona nchini Misri amefariki dunia, na kufanya Afrika kuwa na kifo cha kwanza cha mtu aliyeugua homa hiyo.
Mtalii huyo aliwasili nchini Misri wiki moja iliyopita na kulalamika kuwa na homa kali, na baada ya vipimo aligundulika kuwa na virusi vya corona.
Katika taarifa yake ya hivi karibuni, Wizara ya Afya ya Misri imeeleza kuwa idadi ya watu wanaogua homa ya corona nchini humo imefikia 48.