Saanya kuamua mtanange Jumapili

0
474

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza mwamuzi Martin Saanya kutoka mkoani Morogoro kuwa ndiye atakayeamua mtanange wa watani wa jadi Yanga na Simba utakaofanyika machi nane mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dares salaam.

TFF imemtaja mwamuzi msaidizi namba moja kuwa ni Mohamed Mkono kutoka mkoani Tanga, mwamuzi msaidizi namba mbili ni Frank Komba wa Dar es salaam na mwamuzi wa akiba atakuwa ni Elly Sasii naye kutoka Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa watani wa jadi pia kutakuwa na waamuzi wasaidizi wa ziada ambao ni Abdallah Mwinyimkuu kutoka Singida na Ramadhani Kayoko wa Dar es salaam, huku mtathmini wa waamuzi akiwa Sudi Abdi wa mkoani Arusha na kamishna wa mchezo atakuwa Mohamed Mkweche wa Dar es salaam.