Ghana yasherehekea miaka 63 ya uhuru

0
589

Raia wa Ghana, leo wanasherehekea miaka 63 ya uhuru wa Taifa hilo.

Ghana ilitawaliwa na Uingereza na kupata uhuru wake chini ya Rais Kwame Nkurumah Machi 6, 1957.

Ghana ilikuwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kupata uhuru wake chini ya mwanasiasa huyo mashuhuri Nkurumah na ilijitahidi kuzipigania nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania kupata uhuru wake.

Nkurumah alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Ghana baada ya uhuru na baadae kuwa Rais wa Taifa hilo.

Mojawapo ya kauli alizowahi kusema Kwame Nkurumah katika kusaidia nchi nyingine za Afrika kuondokana na ukoloni ni “Ninauhakika kuwa ni hatari kwa nchi huru za Afrika kungojea muda mrefu ili Uingereza ifanye kazi yake. Wakati umefika wa nchi huru za Kiafrika kuchukua hatua kwa mikono yao wenyewe.”

Shamrashamra za kuadhimisha siku hii ya Uhuru zitafanyika leo, katika Ukumbi wa ‘Baba Yara Sports Stadium’ uliopo Kumasi, mji mkuu wa Mkoa wa Ashanti nchini Ghana huku kauli mbiu ya mwaka 2020 ikiwa ni “Kuunganisha faida zetu.”

Ghana ambayo hapo awali ilijulikana kama ‘Gold Coast’, iliwavutia zaidi wakoloni kwa umaarufu wake wa kuwa na madini ya Dhahabu na pembe za ndovu.

Nyerere pamoja na Nkurumah walifanikiwa kuzipatia nchi zao Uhuru bila kumwaga damu.