Mbunge mwingine wa CUF ahamia CCM

0
234

Mbunge wa jimbo la Ole lililopo Chakechake mkoa wa Kusini Pemba kupitia Chama Cha Wananchi ( CUF) Juma Hamad Omari ametangaza kujivua vyeo vyake vyote ndani ya chama hicho na kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Juma Hamad Omari ametangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa CCM wilayani Chakechake na kupokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

Wakati wa mkutano huo, Wanachama wengine 564 kutoka vyama vya CUF na ACT Wazalendo nao wametangaza kuhamia CCM.

Juma Hamad Omari anakua Mbunge wa pili kutoka CUF huko Pemba kutangaza kukihama chama hicho ndani kipindi cha siku mbili, ambapo hapo jana Mbunge wa Wawi mkoa wa Kusini Pemba, – Ahmed Juma Ngwali alitangaza kuhamia CCM.