Rais Dkt. Shein aitaka skuli ya sheria Zanzibar

0
175

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuna haja ya kuanzishwa kwa skuli ya sheria visiwani humo ili kuimarisha sekta hiyo.

Dkt. Shein ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati ilipowasilisha Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Aidha, Rais Dkt. Shein ameutaka uongozi wa wizara hiyo kuimarisha uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.