Viongozi wa serikali watembelea reli ya SGR

0
163

Makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu kutoka wizara zote wakiangalia handaki namba mbili ambalo linaendelea kukamilishwa ujenzi wake, wakati wa ziara yao kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR, leo Machi 2.

Handaki hilo ni moja kati ya mahandaki manne yatakayopitisha treni za SGR chini ya milima.

Kazi ya ujenzi bado inaendelea kwa kasi katika kipande cha pili cha mradi, kilichotembelewa na viongozi hao kutoka Morogoro hadi Makutupora na hadi sasa asilimia ishirini na nane imeshakamilika.