Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika kituo cha pamoja cha forodha cha Horohoro kudhibiti upimaji wa wageni wanaoingia kutoka nje ya nchi.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Machi 2, 2020 mara alipotembelea kituoni hapo ili kujionea utendaji kazi unavyokwenda, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Tanga.
Kauli ya waziri mkuu imekuja wakati serikali ikiendelea kuchukua hatua madhubuti za kuwapima afya wageni wote wanaingia nchini ili kudhibiti magonjwa mbalimbali kama vile homa ya virusi vya corona, ambayo imekuwa tishio duniani, na ebola.
Na Bertha Mwambela, Tanga