Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo Dkt, Hassan Abbas amesema serikali itaendelea kutetea haki za binadamu katika Nyanja mbali mbali
Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini, DKT ABBAS amesema tarehe 25 mwezi uliopita Tanzania imewasilisha ripoti yake ya haki za binaadamu katika Baraza la Umoja wa Mataifa kilichofanyika GENEVA USWISS na kufanikiwa kutetea nafasi yake
Aidha anabainisha kuwa miradi mingi mikubwa inayotekelezwa nchini Ukiwemo wa Reli ya mwendo kasi SGR unakwenda kwa kasi
Makatibu Wakuu wote watakuwa na ziara ya siku mbili ya kimkakati kutembelea mradi wa Reli wakianzia Dodoma hadi Morogoro kuanzia kesho.