FFU yatakiwa kutenga eneo Dodoma kwa ajili ya mafunzo

0
195

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Simon Sirro amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Paul Sanga kuhakikisha anatenga eneo maalum jijini Dodoma litakalotumiwa na askari wa kikosi hicho kwa ajili ya mafunzo.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la polisi ambalo sasa linatumika kama Makao Makuu ya FFU.

Kwa upande wake Kamanda Sanga amemuhakikishia IGP Sirro kuwa watatekeleza maelekezo aliyowapatia.