Morocco yaomba kuandaa michuano mikubwa Afrika

0
424

Shirikisho la Soka la Morocco limeomba kuandaa fainali za michuano miwili mikubwa ya ngazi ya vilabu barani Afrika ambazo ni Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

Morocco inataka mchezo wa fainali ya mabingwa uchezwe kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo jijini Casablana, na mchezo wa kombe la shirikisho uchezwe kwenye uwanja wa Moulay Abdelahh ulioko mjini Rabat.

Ombi hilo la Morocco la kutaka kuandaa fainali hizo za michuano miwili mikubwa limewasilishwa kwa maandishi na shirikisho la soka la nchi hiyo kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Morocco inakuwa nchi ya pili kuomba kuandaa ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho barani Afrika, baada ya Afrika Kusini kufanya hivyo.

Mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho utachezwa Mei 24 mwaka huu na ule wa ligi ya mabingwa utachezwa Mei 29, na hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi moja kuandaa fainali hizo baada ya CAF kubadili mfumo wa michezo ya fainali kuchezwa nyumbani na ugenini.