Liverpool yaonja kipigo Ulaya

0
359

Liverpool wakiwa ugenini Madrid wameonja uchungu wa kufungwa baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya 16 bora

Bao pekee la Madrid limefungwa na mchezaji Niguez, Liverpool ambao ni mabingwa watetezi watasubiri hadi jumatano ya Machi 11 kujua hatma yao watakapocheza mchezo wa marejeano Anfield

Katika mchezo mwengine Erling Halaand amekuwa mwiba kwa lango la PSG baada ya kutundika mikwaju miwili nyavuni dhidi yao huku Borrusia Dortmund ikiondoka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 wakiwa dimba la nyumbani katika mchezo wa awali wa ligi ya mabingwa Ulaya