Rais Magufuli ateua viongozi watatu

0
1868

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watatu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, uteuzi ambao ulianza rasmi Januari 30 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo walioteuliwa ni Dkt. Benson Otieno Ndiege ambaye amekuwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

Wengine walioteuliwa ni, Mulande Charles Msolwa, ambaye amekuwa Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania-Uhamasishaji na Uratibu, na Nyakunga Collins Bernedict ambaye amekuwa Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania-Ukaguzi na Usimamizi.