Madiwani 5 kutoka ACT Wazalendo wahamia CCM

0
373

Madiwani watano wa Chama cha ACT Wazalendo wamejiuzulu nyadhifa zao zote katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wamepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa kuwapokea wanachama hao wapya, Dkt Bashiru amesema kuwa Madiwani hao walikuwa wa kata za Kasingiriwa, Kagera, Kasimbu, Kipampa na Gungu zote za Manispaa ya Kigoma-Ujiji.

Madiwani hao Hamduni Nassoro wa kata ya Kasingiriwa, Ismail Mahmoud wa kata ya Kagera, Fuad Seif wa kata ya Kasimbu, Mussa Ngongolwa wa kata ya Kipampa na Hamisi Rashidi wa kata ya Gungu, wametangaza uamuzi huo katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.