Watanzania maarufu zaidi katika mtandao wa Instagram

0
1406
Diamond Platnumz: Mwanamuziki anayepeperusha bendera ya Tanzania nchi za nje.

Matumizi ya mitandao ya kijamii yanazidi kubadilika siku hadi siku. Kutoka katika matumizi binafsi ya watu kutuma picha hadi kufikia kutumika kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, kiuhamasishaji na kukuza chapa (brands)/majina.

Instagram ni mtandao unaotumika zaidi katika kufanya shughuli hizi kwa kuwa na akaunti binafsi, za makampuni na wajasiriamali.

Kwa dunia nzima mchezaji wa mpira wa miguu wa timu ya Juventus Ronaldo ndio mtu mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye akaunti yake binafsi iliyothibitishwa na Instagram, akiongoza kwa kuwa na wafuasi 203M.

Kwa upande wa Tanzania wapo watu maarufu wanaotumia akaunti zao za Instagram kujitambulisha kwa shughuli mbalimbali wanazofanya.

Hawa ni watanzania 10 wenye wafuasi wengi zaidi Instagram kwenye akaunti zilizothibitishwa na Instagram (verified).

Diamond Platnumz
Mwanamuziki wa kiume anayepeperusha bendera nchi za nje, mfanyabiashara na baba wa watoto wanne akiongoza kwa kuwa na wafuasi 8.6M

Millard Ayo: Mtangazaji na mmiliki wa AyoTV

Millard Ayo
Muandishi wa habari, mmiliki wa AyoTV na mtangazaji anashika nafasi ya pili kwa kuwa na wafuasi 6.5M

Wema Sepetu
Nafasi ya tatu inaenda kwa mwanadada mfanyabiashara na aliyekuwa Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu kwa wafuasi 6.4M

Vanessa Mdee
Mwanamuziki na mwanamitindo anayepeperusha bendera ya Tanzania kwa kazi zake, pia aliwahi kuwa mtangazaji akiwa na wafuasi 5.9M

Jokate Mwegelo
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni mwanamitindo na aliwahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006 na kujihusisha na utangazaji anashika nafasi ya tano kwa kuwa na wafuasi 5.7M

Jokate Mwegelo: Mkuu wa Mkoa Kisarawe

Jacqueline Wolper
Muigizaji wa filamu za kitanzania anaejihusisha na ubunifu wa mavazi na video vixen ana wafuasi 5.6M

Hamissa Mobetto
Mwanamitindo, muigizaji na muimbaji aliyeanza kujulikana kupitia ‘After School Bash’. Pia ni mama wa watoto wawili naye anashika nafasi ya saba akiwa na wafuasi 5.4M

Shilole
Ni mwanamuziki, muigizaji, mjasiriamali katika sekta ya chakula na mama wa watoto wawili huku akiwa na wafuasi 5.4M

Shilole: Muigizaji na mjasiriamali

Auntyezekiel
Muigizaji wa filamu za bongo, mfanyabiashara ambaye pia alishiriki katika shindano la Miss Tanzania 2006. Auntyezekiel ni mama wa mtoto mmoja na ana wafuasi 5.2M

Ali Kiba
Orodha hii inafungwa na mwanamuziki wa kizazi kipya Tanzania na mchezaji wa mpira wa miguu akiwa na wafuasi 5M

Je! Kuna mtu aliyeachwa? Ni nini maoni yako juu ya orodha hii?