Mahakama nchini Zimbabwe imeamuru kuondolewa nchini humo kwa raia 21 wa Uganda, kwa madai kuwa wameingia nchini humo kinyume cha sheria.
Watu hao walikamatwa Februari 8 mwaka huu wakiwa safarini kuelekea kwenye mji wa Bulawayo, ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe.
Taarifa ya Serikali ya Zimbabwe imesema kuwa, raia hao wa Uganda waliwakwepa maafisa uhamiaji wakati wakiingia nchini humo kutoka Zambia kupitia mpaka wa Victoria.
Licha ya mahakama kuwahukumu watu 20 kati ya hao kifungo cha miezi mitatu jela kila mmoja, ilifuta adhabu hiyo kwa maelekezo kuwa wasitende tena kosa kama hilo ndani ya kipindi cha miaka mitano.