JPM amfukuza kazi aliyechana Quran

0
242

Rais John Magufuli ametangaza kumfukuza kazi mara moja mtumishi wa serikali, aliyechana Quran wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi wa kumfukuzisha kazi Daniel Maleki wakati akizindua rasmi wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, ambapo pia amezindua jengo la utawala la mkuu wa wilaya, jengo la halmashauri na majengo ya hospitali ya wilaya hiyo.

Wakati akisema hayo, Rais amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo kuandika barua ya kumfukuza kazi mtumishi huyo ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi.

“Juzi nilikuwa namsikia Waziri Jafo, yupo mtu mmoja kule Kilosa alichana kitabu Kitakatifu, nakushukuru umechukua hatua ya kumsimamisha kazi, lakini namfukuza moja kwa moja muandikie barua ya kuondoka moja kwa moja, ashinde kesi asishinde huyo sio mfanyakazi wa serikali, hatuwezi kukaa na wafanyakazi wapumbavu”, amesisitiza Rais Magufuli.