Wagonjwa wa Corona waongezeka Marekani

0
385

Raia mmoja wa kimarekani akutwa na virusi vya corona hivyo kuongeza idadi ya wamarekani walioambukizwa kufikia 13 na tayari wamewekwa chini ya uangalizi maalum.

Raia huyo alipatwa na virusi hivyo wakati akiwa San Diego chini ya uangalizi wa siku 14 baada ya kuwasili kutoka China Februari 5.

Rais Donald Trump amesema anaamini kuwa msimu wa majira ya joto unaokuja utasaidia sana kumaliza kabisa mlipuko wa virusi hivyo.