Nimeombwa nirudi Simba: Kocha Uchebe

0
1696

Aliyekuwa kocha wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Patrick Aussems amesema ameguswa na jumbe ambazo ametumiwa na watu wakimuomba arejee msimbazi kuinoa klabu hiyo.

Katika ujumbe alioandika kupitia ukurasa wake wa Twitter, Aussems amesema kuwa Simba ni klabu kubwa na anaitakia kila la kheri, huku akiamini ipo siku atarejea.

“Nimeguswa sana na maelfu ya jumbe nilizopokea kwa siku za karibuni nikiombwa kurejea. Simba ni klabu kubwa, yenye wachezaji wazuri, na mashabiki bora. Nawataki kila la heri, na ninaamini siku moja tutaonana tena,” amesema kocha hiyo maarufu kwa jina la Uchebe.

Simba ilivunja mkataba na kocha huyo Disemba 2019 kwa kile ilichosema ni makosa ya nidhamu baada ya kocha huyo kwenda Afrika Kusini bila kutoa taarifa.

Simba ilimteua Mbelgiji Sven Vanderbroeck kushika nafasi hiyo.