Donge nono kutolewa kwa atakayegundua kinga ya Corona

0
412

Nyota wa filamu za kichina, Jackie Chan ametangaza donge nono la Yuan milioni moja (wastani wa milioni 330 za kitanzania) kwa yeyote atakayegundua kinga au tiba dhidi ya virusi vya Corona.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Weibo, Chan amesema kuwa yupo tayari kufanya chochote kuona virusi vipya vya Corona vikipatiwa tiba, kujulikana chanzo na kutokomezwa.

Kufuatia hatua hiyo, Chan amepokea pongezi kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Tayari virusi hivyo vya Corona vimesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja nchini China.