Waziri wa TAMISEMI afuta vibali vya safari za viongozi

0
682

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amepiga marufuku wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri kutoka nje ya vituo vya kazi kwenda kuhudhuria mikutano, semina na warsha mbalimbali na pia amefuta vibali vyote vilivyotolewa kwa ajili ya safari hizo.