Equatorial Guinea kuisaidia China kupambana na Corona

0
317

Serikali ya Equatorial Guinea imetangaza kuipatia China msaada wa Dola Milioni Mbili za Kimarekani, kwa ajili ya kuwezesha mipango ya kukabiliana na virusi vya Corona.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana hivi karibuni na kuongozwa na Rais Obiang Nguema Mbasogo.

Equatorial Guinea imeeleza kuhuzunishwa na hali iliyopo nchini China, nchi ambayo ni mshirika wake mkubwa.

China imewekeza katika sekta mbalimbali huko Equatorial Guinea zikiwemo zile za mawasiliano ya simu, miundombinu na teknolojia.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeeleza kuwa, hadi sasa virusi hivyo vya Corona vimeathiri zaidi ya watu Elfu 24 nchini China huku vifo vikiwa ni 490.