Mwamposa na wenzake waachiwa kwa dhamana

0
373

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limemuachia kwa dhamana ‘Mtume’ Boniface Mwamposa na watu wengine saba waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuandaa kongamano lililopelekea vifo vya watu 20 na wengine 16 kujeruhiwa.

Mwamposa alikamatwa jijini Dar es Salaam Februari 2 mwaka huu akitaka kutoroka, baada ya tukio hilo kutokea katika Uwanja wa Majengo, mjini Moshi.

Watu hao walifariki dunia na kujeruhiwa wakati wakigombania kukanya mafuta yanayodaiwa kuwa na upako yanayotolewa na kiongozi huyo wa kidini.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi iliyotolewa Februari 3, tayari watuhumiwa hao wamehojiwa, na polisi wanaendelea na uchunguzi, na kwamba hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa endapo itabainika kuna kosa la jinai lililosababisha vifo na watu kujeruhiwa.