JPM atuma Salamu za Pole

0
158

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa Rais Uhuru Kenyatta na Wakenya wote kufuatia kifo cha Rais Mstaafu, Daniel Arap Moi.

Rais Magufuli ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa twitter

Rais Magufuli amesema Watanzania watamkumbuka Rais Moi kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya, na kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki.