Watumishi wa TANESCO waagwa Mbogwe katika Uwanja wa Shule ya msingi Masumbwe

0
661

Watumishi wanne wa shirika la umeme nchini TANESCO waliofariki katika ajali ya gari juzi, Februari 1, wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wameagwa leo katika viwanja vya shule ya msingi Masumbwe.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameongoza watumishi wa wizara hiyo, wafiwa na watumishi wa TANESCO na kusema, wafanyakazi hao walikuwa wachapa kazi na wameacha alama wilayani Mbogwe kwa utendaji wao wa kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewataka wafiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki na waendelee kumtumainia Mungu kwa kuwa ndiye mfariji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO nchini Dkt. Tito Mwinuka amesema shirika hilo limepata pigo kubwa, kupoteza watumishi wanne kwa wakati mmoja haijawahi kutokea.

Watumishi waliofariki ni; aliyekuwa meneja wa TANESCO wa wilaya ya Mbogwe Weston Jafu, dereva Laiki John, fundi sanifu, Joshua Silanga na fundi mchundo Saumu Bwesa na miili ya marehemu itasafirishwa katika mikoa ya Dodoma, Simiyu, Mbeya na Songwe.

Nazareth Ndekia, TBC Mbogwe Geita