Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesitisha huduma na matumizi ya nakala za mtandaoni za kitambulisho cha taifa (online ID copy) iliyokuwa inapatikana kwenye tovuti yake na badala yake kubakiza huduma ya kupata namba ya kitambulisho tu.
NIDA imesema hayo katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Januari 30 mwaka huu, lakini haijaeleza sababu za kusitisha huduma na matumizi ya nakala hizo.
Awali mtu ambaye tayari amejiandikisha na taarifa zake kuchakatwa, au aliyepoteza kitambulisho aliweza kupata nakala ya mtandaoni kwa kujaza taarifa za msingi kama vile majina yake, namba yake, taarifa za wazazi, na eneo alipojiandikishia.