Serikali yaboresha utoaji huduma za afya Kilimanjaro

0
225

Serikali kupitia hospitali ya rufaa ya Mawenzi iliyopo Mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kuboresha huduma za afya kutokana na kuwekeza wataalam pamoja na vifaa tiba hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Timu ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Jumanne Karia amesema kuwa utoaji wa huduma umeimarishwa kutokana na upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na wataalam katika maeneo mbalimbali.

Katika uboreshaji huo wameongeza vitanda hadi kufikia 300 na kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa asiliamia 100.

Aidha katika kipindi cha miaka minne ya Rais John Magufuli hospitali hiyo imefanikiwa kufanya upasuaji wa kuondoa ukungu wa jicho kwa wagonjwa 640 pamoja na kupandikiza kioo cha jicho kwa wagonjwa watatu.