Hospitali yajengwa China kudhibiti virusi vya Corona

0
332

Ikiwa idadi ya vifo vinavyosababishwa na virusi hatari vya Corona inaongezeka, nchi ya China imeanza ujenzi wa hospitali maalum kwaajili ya waathirika wa virusi hivyo.

Ujenzi huo ulioanza Januari 23, bado unaendelea huku ukitarajiwa kukamilika rasmi Februari 5.

Serikali ya China imeripoti kuwa hadi sasa kuna vifo 80 nchini humo huku takribani kesi 2800 zimeripotiwa duniani.

Tukiacha China, Korea Kusini, Japan, Thailand, Ufilipino, Hong Kong, Malaysia, France, Australia, Marekani na Canada ni baadhi pia ya nchi zinazosumbuliwa na virusi hivyo.