Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka wabunifu wa Tanzania kuhalalisha kazi zao za mitindo ili kupata furusa mbalimbali zinazopita kwenye wizara kutokana na kujulikana na kutambulika na serekali kihalali.
Mhe. Shonza ametoa wito huo wakati alipotembelea kiwanda kidogo cha kushona nguo cha mbunifu wa mavazi Ally Rehmtullah muda mfupi baada ya kuzindua rasmi duka la bidhaa za ubunifu wa mavazi la mbunifu huyo mkongwe leo tarehe 25/01/2020 lilopa Masaki jijini Dar es Salaam.
Duka la Ally Rehmtullah litakuwa ni kituo (Fashion HUB) kwa ajili ya wabunifu wote kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Kituo hicho ni sehemu ya wabunifu ambao hawana ofisi kukutana na wateje wao mbalimbali na kujiajiri kutokana na uwepo wa mafundi na sehemu kubwa.
Duka la Ally Rehmtullah jipaya lina “Wi-Fi” ya bure ili kuwapa wabunifu nafasi nzuri ya uwezekano wakuuza vitu mtandaoni na kunitangaza zaidi kama njia yakurasimisha usasa uliopo katika biashara ya ubunifu wa mavazi duniani.