Barrick waingia makubaliano na serikali ya Tanzania

0
284

Serikali imesaini mikabata tisa na Kampuni ya Madini ya Barrick mapema leo hii Ikulu, jijini Dar es Salaam mbele ya Rais Magufuli baada ya majadiliano kati ya pande hizo mbili yaliyoanza tangu mwaka 2017.

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Madini ya Barick (Barrick Gold) ni pamoja na kuanzishwa kwa kampuni mpya ya pamoja ya kusimamia masuala ya madini Twiga Minerals Cooperation.

Waliosaini mikataba hiyo ni pamoja na; Waziri wa Madini Doto Biteko, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Paschal Malata, Msajili wa Hazina (TR) Athumani Mbutuka, na Kamishna Msaidizi wa Madini Terence Ngole.

Baadhi ya mikataba iliyosainiwa ni pamoja na:

Mkataba wa msingi wa makubaliano.
Mkataba wa menejimenti na utoaji wa huduma.
Mkataba wa wana hisa wa Twiga Mineral Corporation.
Mkatabba wa wana hisa wa North Mara.
Mkataba wa wanahisa wa kampuni ya Bulyanhulu.
Mkataba wa wanahisa wa kampuni ya Buzwagi.
Mkataba wa maendeleo wa mgodi wa North Mara.
Mkataba wa maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu.
Mkataba wa maendeleo wa mgodi wa Pangea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikaino wa Afrika Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi, amesema mikataba hii ina maslahi kwa pande zote mbali.