Kusheheni kwa makundi ya nzige kwaleta hofu ya uhaba wa chakula Afrika Mashariki

0
390

Janga la kuwepo kwa nzige limepamba moto katika baadhi ya nchi ukanda wa mashariki mwa Afrika, huku wananchi wakihofia kutokea kwa uhaba wa chakula.

Nzige hao wa jangwani wametapakaa katika baadhi ya sehemu nchini Kenya ikiwemo Meru, Isiolo na Majir na kusababisha uharibifu wa mazao na hofu ya njaa endapo uharibufu huu utaendelea.

Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Chakula Duniani (FAO) wameingilia kati kusaidia nchi ya Kenya kuondokana na janga hili, huku wakisema kuwa njia pekee ya kupambana na kundi kubwa namna hii ni udhibiti wa angani ambao umeshaanza rasmi katika sehemu zilizoshambuliwa

Nchi nyingine kama Uganda, Sudan na Ethiopia , zimeanza pia kushambuliwa na nzige hawa, huku wataalamu wakisema, kuna uwezekano wa nzige hao kuendelea kusambaa na kuzaliana zaidi kutokana na hali ya hewa ya sasa.