China kudhibiti virusi vya Corona

0
431

Rais Xi Jingping wa China amesema serikali yake ipo mbioni kudhibiti kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya aina ya Corona.

Ping amesema maisha ya watu na afya zao zinapaswa kupewa kipaumbele cha juu ambapo tayari wameanza kuwafanyia uchunguzi wasafiri wote wanaoingia na kutoka nchini humo.

Tayari maafisa wa afya wamethibitisha kuwa ugonjwa huo ni wa kuambukiza kwa njia ya kukaribiana au kugusana ambapo hadi sasa jumla ya kesi 217 za waathirika wa virusi hivyo zimethibitishwa katika mji wa Wuhan , Beijing na Shanghai huku watu wanne wakiripotiwa kufa.

Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO imesema itakutana na wataalamu wa afya wiki hii kujadiliana jinsi ya kupatia ufumbuzi ugonjwa huo uliosambaa nchini china.

Virusi vya Corona vinahusishwa na ugonjwa wa SARS unaosababisha tatizo la kupumua ambapo mnamo mwaka 2002 /2003 uliuwa watu 650 nchini humo.

Picha kuu: Reuters