Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Salehe Mhando ameagiza kusakwa kwa viongozi wanaodaiwa kuwa ni wa serikali, wanaokodisha maeneo ya hifadhi na ushoruba wa wanyamapori kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo, ufugaji, uwindaji, na wengine kufanya makazi katika maeneo hayo.
Operesheni hiyo imefanyika kwa kushirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama mkoani Katavi, ambapo waliokamatwa katika hifadhi hizo wamesema wamekuwa wakikodishiwa maeneo hayo na viongozi wa serikali za vijiji.
Mhando ameamuru wahusika wote wasakwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.