Samatta Kutua Aston Villa

0
576

Timu ya Aston Villa ya England inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mtanzania Mbwana Samatta kwa dau la pauni Milioni kumi sawa na bilioni 30 za kitanzania.

Samatta ni chaguo namba moja la kocha wa Aston Villa Dean Smith katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwenye kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania amekuwa kivutio kikubwa kwa timu za England tangu afunge goli kwenye mchezo waligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Liverpool.

Taarifa za kina zinasema hivi sasa pande mbili za timu hizo ziko kwenye mazungumzo ya mwisho ili kukamilisha usajili huo na kocha wa Aston Villa anaonyesha kumtaka sana Samatta ili kuziba nafasi ya mshambuliaji wa Kibrazil Wesley ambae ni majeruhi.

Hata kama usajili huo utakamilika leo au kesho Mbwana Samatta hataweza kucheza mchezo ujao wa ligi ya dhidi ya Brighton kwasababu atakuwa bado hajakamilisha vibali vya kufanya kazi lakini itakuwa habari njema kwake kwasababu itakuwa ametimiza ndoto yake ya kucheza England.