Karia ateuliwa kuratibu fainali za AFCON 2021

0
606

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad kazi yake ni kuratibu fainali hizo.

Mbali na Wallace Karia, Watanzania wengine wawili wameteuliwa kuingia kwenye kamati za CAF akiwepo Dkt. Paul Marealle ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya tiba na Lina Kessy aliyeteuliwa katika kamati ya mpira wa miguu wa wanawake.