Viongozi wa Libya washindwa kufikia makubaliano ya amani

0
380
Meza ya mazungumzo ya amani ya Libya yaliyofanyika jijini Moscow, Urusi. [Picha: EPA]

Kiongozi wa kikundi cha waasi cha kijeshi nchini Libya, Jenerali Khalifa Haftar ameondoka jijini Moscow bila kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya kikosi chake na serikali ya nchi hiyo.

Urusi na Uturiki Jumatatu, Januari 13, zilikutana na kufanya mazungumzo kwa muda zikiwashawishi Jenerali Haftar na Waziri Mkuu wa Libya, Fayel al-Sarraj kumaliza mapigano ambayo yamedumu kwa miezi tisa sasa.

Serikali ya Libya inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN), waziri wa mambo ya nje wa Urusi amethibitisha.

Waziri huyo alisaini makubaloano hayo ya kuweka silaha chini na kumaliza mapigano, lakini Haftar aliomba kuongezewa muda hadi Jumanne asubuhi ili apitie nyaraka za makubaliano kabla hajasaini.

“Makubaliano yameacha matakwa mengi ya viongozi wa kijeshi wa Libya,” amesema Haftar kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Al Arabiya.

Vikosi vyake vimekuwa vikishambulia mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli ambao bado upo mikononi mwa serikali.