Diamond na Eto’o kujenga shule ya soka Tanzania

0
572
Mwanamuziki Diamond Platnumz (kulia) akiwa na nyota wa soka Samuel Eto'o (kulia)

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema kuwa amefanya mazungumzo na nyota wa soka kutoka nchini Cameroon, Samuel Eto’o kwa ajili ya kujenga shule ya mafunzo ya mpira wa miguu nchini Tanzania.

Diamond ameyasema hayo siku chache baada ya kutumbuiza katika hafla ya utoaji wa tuzo za soka Afrika zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) nchini Misri.

Amesema kuwa anataka kufanya hivyo kwa sababu Afrika Mashariki kuna vipaji vingi sana vya soka.

“Kipindi cha nyuma niliona kama kuingia kwenye sekta ya michezo ni biashara isiyo na faida, lakini sasa naona kuwa ina faida. Siku za karibuni nitakuwa na timu yangu ambayo tayari ipo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa sababu sitaki kuanzia chini,” amesema Diamond.

Mwanamuziki huyo hajabainisha kuwa ni lini mipango hiyo itakamilika, lakini amesema uamuzi ambayo tayari ameufanya ni kununua timu ambayo tayari ipo au kununua wachezaji wakubwa.