TFS yatakiwa kuweka miundombinu rafiki kwa walemavu

0
244

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, wenye Ulemavu Stellah Ikupa ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Wamiliki wa Mahoteli kuweka mazingira bora kwa ajili ya Walemavu.

Ikupa ameyasema hayo wakati anazungumza na waandishi wa Habari wakati wa ziara ya chama cha wabunge wenye ulemavu katika Mji Mkongwe wa Bagamoyo.

Aidha anaipongeza TFS kwa huduma wanayoitoa pamoja na jukumu jipya walilopewa la kusimamia Mali Kale.