Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuboresha usikivu wa redio katika maeneo yenye changamoto za usikivu mkoani Kilimanjaro.
Sambamba na hilo, Dkt Mwakyembe pia amesema kitendo cha (TBC) kuagiza vifaa katika baadhi ya vituo mkoani humo kutasaidia wananchi kupata matangazo ya TBC bila usumbufu wowote.
Dkt Mwakyembe yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku mbili ya kuangalia usikivu wa TBC pamoja na changamoto zinazovikabili vituo hivyo.