TMA yatoa tahadhari ongezeko la Joto maeneo ya Pwani

0
172

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakua na ongezeko la joto katika baadhi ya maeneo nchini kufuatia kuwepo kwa hali ya unyevunyevu angani.

Ukanda wa pwani hususani maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba unatarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha joto cha kati ya nyuzi joto 32 hadi 34.