Samaki auzwa billioni nne za kitanzania mnadani.

0
342
Kiyoshi Kimura akionesha samaki aliyemnunua kwenye mnada huko Tokyo, Japan

Mpishi mashuhuri nchini Japan Kiyoshi Kimura maarufu kama ‘Sushi King’ ameweza kuibuka kinara katika mnada mkubwa wa samaki duniani huko Tokyo, Japan.

Katika soko la samaki la Toyosu, Kimura alinunua samaki aina ya Bluefin Tuna mwenye pounds 608 sawa na 276kg kwa takribani dola milioni moja nukta nane ($1.8m) sawa na shillingi billioni 4,141,440,000 za kitanzania.


Mnada huu wa samaki ndio mnada mkubwa wa kufungulia mwaka ambapo samaki anayeuzwa kwenye anakuwa ndio samaki mwenye bei kubwa zaidi ya samaki watakaouzwa kwenye minada yote itakayofuata mwaka mzima.


Aina hii ya samaki wa Bluefin Tuna wanasadikiwa kuwa na uwezo wa kuishi hadi miaka arobaini.


Samaki huyu aliyeuzwa Januari 05, ameshika record ya pili ya samaki aliyeuzwa kwa bei kubwa tangu minada hii kuanza miaka ya 1990 baada ya Kimura kununua samaki wa aina hii mwenye 278kg mwaka jana kwa dollar millioni 3.1 za kimarekani.

Picha kuu: Kiyoshi Kimura akionesha samaki aliyemnunua kwenye mnada huko Tokyo, Japan.
Picha: Takashi Aoyama/Getty Images