Kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu Alfred Ngalariji ameita kikosi cha wachezaji 17 wanaounda timu ya taifa ya mchezo huo itakayoshiriki michuano ya awali ya kufuzu kwa michuano ya mataifa ya Afrika baadae mwaka huu.
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji watatu wanaocheza mpira wa kulipwa nchini Uganda
Ametaja wachezaji wanaounda timu hiyo kuwa ni pamoja na Musa Chacha wa JKT, Stephano Mshana wa VBC, Kaikai Leka wa Savio, Sudi Ulanga anacheza Uganda, Baraka Sadick wa JKT, Erick John wa Oilers na Ally Mohamed wa JKT.
Wachezaji wengine ni pamoja na Enericko Augustino wa ABC, Cornelius Peter wa Savio, Ladslaus Lusajo wa Eagles, Amin Makosa wa Uganda na Isaya Aswile wa Mbeya Flames.
Wengine ni Fadhili Chuma wa Uganda, Haji Mbegu wa JKT, Mwalimu Heri wa VBC, Jackson Brown wa JKT na Gwalugano John wa VBC
Timu hiyo inaingia kambini kesho Jumanne kuanza maandalizi ya michuano hiyo itakayofanyika Nairobi, Kenya