Vijana watakiwa kuzingatia vyakula na mazoezi

0
239

Akiongoza Misa ya Shukrani katika Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenarali DAVID MSUGURI

Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila amesema siri pekee ya kuishi miaka mingi ni mazoezi na mpangilio bora wa chakula

Amesema Vijana wengi kwasasa hawana utaratibu wa kufanya mazoezi hali inayopelekea kuruhusu magonjwa mbalimbali katika miili yao hali inayosababisha kutokuishi kwa muda mrefu

Amewataka Vijana kuzingatia mazoezi na kufanya mpangilio mzuri ili waweze kuishi kwa muda mrefu kama ilivyotokea kwa Jenerali Msuguri